1. Bwana tunakusujudu, Mbele zako twaja, Tunaomba kwa sauti— Je, utaongea?
Tubarikie mfungo Na nafsi ulishe, Ili ukawe na sisi Tufurahi nawe.
2. Tumelisha wahitaji, Maskini twawapa, Tukawalaki wageni— Je, utaongeza?
Tubarikie mfungo Na nafsi ulishe, Ili ukawe na sisi Tufurahi nawe.
3. Kama mashahidi twaja Kukupa shukrani, Kwa kutenda miujiza, Bwana tubariki.