1. Yesu ninapokuwaza Nafurahi mno; Na nitafurahi hasa Nikikaa kwako.
2. Hakuna cha kukumbuka, Wala jina tamu, Jema na lenye baraka, Kama lako Yesu!
3. Kwa wote wanyenyekevu, Huwapa furaha, Mkarimu kwa waovu Wakikurudia!
4. Yesu, u furaha yetu, U zawadi pia, Ndiwe utukufu wetu, Sasa na daima.