Book cover

Sala Tamu

Nyimbo za Dini, 74


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Sala tamu! Sala tamu! Yanirudisha kwa Mungu Nakuwa mbele ya enzi, Nikaseme mahitaji. Ninpopatwa na shida, Nafsi hupata faraja Na kuyakwepa maovu, Irudipo sala tamu! Na kuyakwepa maovu, Irudipo sala tamu!

2. Sala tamu! Sala tamu! Napeleka dua zangu Kwake aliye mkweli Nafsi yangu abariki. Nitafute uso wake, Na nishike neno lake, Nimpe mzigo wangu Ikifika sala tamu! Nimpe mzigo wangu Ikifika sala tamu!