1. Kuna muda mtulivu, Pasipo karaha; Mbele ya Bwana nasali Sala ya faragha.
Moyo na ugeuke, Kuomba siku zote, Na ili nafsi yangu Iungane na mbingu.
2. Njia nyofu ya mbinguni, Wapo malaika, Twaipata tufanyapo, Sala ya faragha.
Moyo na ugeuke, Kuomba siku zote, Na ili nafsi yangu Iungane na mbingu.
3. Dhoruba nipitiapo, Ni faraja kwamba, Bwana husikia ile, Sala ya faragha.
Moyo na ugeuke, Kuomba siku zote, Na ili nafsi yangu Iungane na mbingu.
4. Adui anitegapo, Mwokozi namwita, Huja kama nitasali, Sala ya faragha.