Book cover

Kwa Upole Twaimba

Nyimbo za Dini, 78


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Kwa upole twaimba, Sabato yaja tena. Tupumzike, Tupumzike, Na tushukuru Mungu Baraka atupaye, Baraka atupaye.

2. Ndiyo siku teule, Mungu tumtafute, Ni thawabu, Ni thawabu, Na tule sakramenti Kumkumbuka Yesu, Kumkumbuka Yesu.

3. Tuongeze sauti Tuletapo zawadi Ya upole, Ya upole, Kama dhabihu yetu Ni kwa neema yake, Ni kwa neema yake.

4. Ni mtukufu Kristo; Ni zuri lake neno: Fanya toba, Fanya toba; Japo dhambi nyekundu, Msamaha atoa. Msamaha atoa.