1. Kama umande wa mbingu Ushukavyo nyasini Ili kuzitia nguvu Pamoja na ulinzi,
2. Hivyo mafundisho, Bwana, Yashuke toka kwako, Yaweze kutosheleza Kaziyo ya upendo.
3. Ona waumini, Bwana; Timizia ahadi. Kutoka mbinguni tuma Umande wa uhai.
4. Sikia maombi yetu. Mtume Roho aje, Ili watu wasujudu Pia wakutukuze.