1. Kaa nami! Kwani kumekuchwa; Usiniache gizani, Bwana! Wanaposhindwa wasaidizi, Auni wa kweli, kaa nami!
2. Siku zinayoyoma haraka. Duniani raha hufifia. Naona mabadiliko mengi; Ewe Mwaminifu, kaa nami!
3. Kila saa ninakuhitaji. Nani atamshinda Shetani? Mwimo wangu, mwingine hakuna, Kila hali kaa nami, Bwana!