1. Twapokea sakramenti, Twakugeukia, Ewe Mwana wake Mungu, Uliyetufia. Neema isiyokoma, Nao upendowe, Umetupa na uzima Wa milele yote.
2. Kumbukumbu twarejesha Kuzitubu dhambi; Njia ni utakatifu— Ndivyo uliishi. Msamaha ni zawadi Tunayotafuta. Kwa mikono ya ahadi, Sakramenti twala.
3. Tunakusifu na wimbo, Tunakuabudu. Zitabaki mioyoni Baraka za siku. Tupatie ujasiri Wa kusikiliza. Ee Bwana tunashukuru; Tutakufuata.