1. Ninainamisha kichwa Na kukuwaza Mwokozi. Sakramenti nachukua Kuikumbuka ahadi.
2. Nakusihi nikumbushe Ulinifia Golgotha, Ili nikue milele Niishi na wewe, Bwana.
3. Macho yangu nainua, Kuangalia mbinguni, Ili niweze kujua Nifanyeje kustahili.
4. Niishivyo duniani, Nipe Roho nikaweze Kubadilika moyoni, Na kukua kama wewe.