1. Kwa unyenyekevu, Bwana,Twaomba Roho wako.Twabariki sakramentiKatika jina lako.Mwokozi sitasahauUlivyo sulubiwa,Ulivunjwa moyo wakoJuu ya msalaba.
2. Tuwezeshe kusamehe,Tuwe wavumilivu.Sala zetu zije kwakoJuu patakatifu.Iwapo tutastahili,Dhabihu takatifu,Twakuomba tuwe nawe;Tuwe na utukufu.