Book cover

Ee Baba wa Milele

Nyimbo za Dini, 94


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Ee Baba wa milele,Uliye mbinguni,Katika jina Lake,Takasa, bariki—Ikiwa tu wasafi—Mkate, divai,Ili tuikumbukeDamu nao mwili.

2. Dhabihu takatifuTusiyoelewa,Kusamehewa dhambi,Na kumkumbuka,Ili tushuhudieKuteswa kwa Kristo,Tuwe na Roho wake,Na upatanisho.

3. Na Yesu, Mteule,Akashuka chiniKujitoa dhabihuKuokoa nafsi—Asiye na mvuto,Wa kutamaniwa—Mwokozi wa ahadiAkatutakasa.

4. Ile hekima kuu,Mpango kamiliUlifanya wokovu,Neno kuwa mwili,Kushuka dunianiAwe mwanadamu,Afe, japo Mfalme,Kutuweka huru.