Book cover

Tunaposhiriki Nembo

Nyimbo za Dini, 95


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Tunaposhiriki nemboKwa jina la Yesu Kristo,Sote na tuihakikiMioyo kama ni safi.

2. Kristo damu alimwaga,Golgotha ilimwagika,Kifungo kutunusuruNa kuepuka adhabu.

3. Hivyo Yesu alikufaIli haki kutimia,Ili watu tuwe huruNa kifo pia kuzimu.

4. Lakini tutafufuka,Na tutaishi daima,Hatutateswa na kifo,Tutatawala na Kristo.