1. Baba yetu twaamini Ahadi za kwako; Tunapokea injili, Wema wasemavyo.
2. Tunatubu zetu dhambi Pia kwako twaja. Agano tunakubali Kuchagua mema.
3. Kubali maombi, Bwana, Na utusamehe, Tukawe viumbe wapya Na dhambi tuache.
4. Sakramenti twapokea Kwa jina la Kristo, Ili tupate mwangaza Kwenye maagano.
5. Kwenye maji twazamishwa Kwa jina la Yesu, Tufufuke na mwangaza Wa Roho wa Mungu.
6. Utubatize kwa Roho, Wana wako tuwe, Tukawe pamoja nao Wateule wote.