1. Alipokuwa mbinguniBwana aliteuliwaKuokoa wenye dhambi;“Iwe upendavyo, Baba.”
2. Mtawala na MfalmeMnyenyekevu akawa,Wakati na hali zote;“Iwe upendavyo, Baba.”
3. Si miiba, si kejeliKristo zingemzuia.Hakujali yake nafsi;“Iwe upendavyo, Baba.”
4. Mkate nacho kikombe,Ni kumbukumbu ya Bwana.Tuombe nguvu tuseme,“Iwe upendavyo, Baba.”