1. Mwokozi uvaaye Taji la miiba, Mateso ubebaye, Ya kebehi kubwa. Wakuputa askari; Wakunywesha nyongo; Juu msalabani Wateswa kwa kifo.
2. Hakuna mwenye dhambi Aliye baniwa, Utukufu kuhisi Na kuokolewa. Wa kusaliti wapo, Wajua pendowe; Nao wakuuao Neema i bure.
3. Dhabihu ya ajabu Imelipa deni; Rehema yako ndefu Ipo duniani. Japo mwovu hudhuru, Tu vitani bado, Sasa hatuna hofu, Twamwamini Kristo.
4. Sifa gani tutoe Kushukuru, Bwana? Msalabani pale Juu ulifia, Kwa mpango wa Mungu Kuokoa nafsi. Kwako mpendwa Yesu, Twaleta hisani.