Book cover

Kafufuka!

Nyimbo za Dini, 111


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Kafufuka! Kafufuka! Itangaze kwa shangwe. Kifungo chake kavunja; Watu wafurahie. Kifo kina ukomo, Ushindi ni wa Kristo.

2. Njoo na utakatifu; Sifu ushindi wake. Hakuna kiza cha wingu Kuzuia miale, Siku njema yaanza, Ishara ya Pasaka.

3. Kafufuka! Kafufuka! Amefungua mbingu. Dhambi haitatufunga, Tuna utakatifu. Na nuru ya Pasaka Machoni itang’aa.