Book cover

Kwenye Mji wa Daudi

Nyimbo za Dini, 115


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Kwenye mji wa Daudi Kwenye zizi la ng’ombe, Ndipo mama kamlaza Horini mwana wake; Mama mpole Maria, Yesu mwanae mchanga.

2. Alikuja duniani, Bwana Mungu wa wote. Kwenye nyasi alilala, Zizi hifadhi yake; Wapole nao maskini, Kristo aliwathamini.

3. Na sote tutamuona Kwa wake ukombozi, Kwani mtoto mpole Ni Mungu wa mbinguni; Huwaongoza watoto Mahali ambapo yupo.