Book cover

Mji Mwema, Bethlehemu

Nyimbo za Dini, 119


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Mji mwema, Bethlehemu,Tuli watulia.Ulalapo, nyota nazoZinapita kimya;Na gizani yang’aaNuru ya milele.Tumaini za vizaziZatimia nawe.

2. Hivyo Kristo azaliwa;Malaika juuWakalinda kwa upendoWakistaajabu.Nyota za alfajiriUjio tangaza,Imbeni sifa kwa Mungu,Kwa watu faraja.

3. Kimyakimya, hivyo ndivyoZawadi hupewa!Mungu atoa kwa watuZa kwake baraka.Hawataona aja;Ila duniani,Kote wapole walipoKristo aja kweli.