1. Bwana, pokea uliko Kila anayetubu, Azaliwaye kwa maji Na roho wako, Mungu. Wafariji na ongoza Maisha ya vijana; Na neno lako tukufu Liwape maarifa.
2. Hamjui ndiye Mungu? Na akawa shahidi, Kwamba njia ni nyembamba Irudiyo mbinguni. Sikia habari njema; “Njoo, unifuate Katika ufalme wangu, Na uishi milele.”
3. Ukweli umerejeshwa: Ibada takatifu, Kwa agano ziokoe Milele wanadamu! Watu wote mfurahi! Watu wote muimbe! Waliokufa wasifu Mungu wetu Mfalme!