1. Ninakupenda, Mwokozi,Napita njia yako.Nitainua wengine,Nipate nguvu kwako.Ninakupenda, Mwokozi—Bwana, kwako naja.
2. Mimi nani kuhukumu?Nami siko kamili.Mioyo kimya hufichaMasononeko mengi.Mimi nani kuhukumu?Bwana, kwako naja.
3. Nitawajali wengine,Nijifunze kuponya.Wahitaji na wanyonge,Nitawahurumia.Nitawajali wengine—Bwana, kwako naja.
4. Nitapenda ndugu zanguJinsi unipendavyo.Uwezo wako nipateNifanye kazi yako.Nitapenda ndugu zangu—Bwana, kwako naja.