1. Wapendwa wa Mchungaji,Ni kondoo wapendwa;Tunu pendo awapalo,Tunu kuliko fedha.Wapendwa wa Mchungaji,Na kondoo “wengine”;Milimani awasaka,Hata kina chochote.
Jangwani watangatanga,Wasumbuka wapweke;Aenda kuwakomboa,Zizini warudishwe.
2. Wapendwa wa Mchungaji,Ndio wanakondoo;Kuna wanaopotea,Wadhoofika huko.Ona, Mchungaji Mwema,Asaka wapotevu,Awarudisha kwa shangwe,Na kwa gharama kuu.
Jangwani watangatanga,Wasumbuka wapweke;Aenda kuwakomboa,Zizini warudishwe.
3. Wapendwa wa Mchungaji,Ni “tisini na tisa.”Apenda wapoteao,Tumaini wakosa.Sikia! Wito wa moyo,Kwa upole asihi:“Hutafuti mpotevu,Aliye mbali nami.”
Jangwani watangatanga,Wasumbuka wapweke;Aenda kuwakomboa,Zizini warudishwe.
4. Malisho yanavutia;Maji yenye uhai.Bwana, kwa ari twajibu,“Ndiyo, tunakubali!Tufanye wachunga wako;Tupe pendo la kina.Tutume mbali jangwani,Kondoo kuwasaka.”
Jangwani watangatanga,Wasumbuka wapweke;Twendeni kuwakomboa,Zizini warudishwe.