1. Kuna lolote jema nimefanya? Kuna niliyemuinua? Kuna mwenye dhiki niliyefariji? La sivyo, nimekosa. Niliondolea mtu vikwazo Kwa kujitolea kwangu? Walipata nusuri wachovu nao? Walipoita, nilijibu?
Amka, fanya zaidi Ya kuota u mbinguni. Tenda jema daima, utafurahia Baraka za maadili.
2. Fursa za kazi zipo hata sasa, Nafasi zatujia tele. Chunga usipitwe, usihairishe, Bali nenda kafanye. Ni uadilifu mtu kutoa; Upendo unathawabu. Mtenda jema, yeye ni msaada. Wema sio bure kwa Mungu.
Amka, fanya zaidi Ya kuota u mbinguni. Tenda jema daima, utafurahia Baraka za maadili.