Book cover

Tuambizane Mema Daima

Nyimbo za Dini, 132


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Tuambizane mema daima Nyumbani au popote; Kama ndege kati ya maua Sauti zipokelewe. Yafariji kwenye majonzi, Yatutia moyo nguvu, Na penye wingu la huzuni, Huleta pendo ng’aavu.

Kila neno jema litatukumbusha, Labakia kama kito. Tuambizane mema daima; Yawa taswira ya moyo.

2. Kama mwale wa jua Sayuni Nafsi yanafurahisha; Kama kisima cha maji safi, Taratibu yatuwama. Hivyo kwa sauti karimu, Urafiki tuujenge, Mioyo iwe mikunjufu Na kufurahi popote.

Kila neno jema litatukumbusha, Labakia kama kito. Tuambizane mema daima; Yawa taswira ya moyo.