1. Tuko huru kuchaguaJinsi tutakavyokuwa;Mungu hatulazimishiKurudi kwake mbinguni.
2. Aita, aelekeza,Abariki kwa mwangaza,Ni mkarimu, mzuri,Na pia halazimishi.
3. Bila uhuru, busara,Sisi ni kama wanyama,Ambao hawafahamuPeponi na jehanamu.
4. Tutumie mamlakaKuchagua yale mema;Anafurahia KristoTukitafuta upendo.