Book cover

Ee Mungu, Angaza

Nyimbo za Dini, 136


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Ee Mungu, angaza Kwa uwezo wako, Kusudi wezesha Lisambazwe neno; Ufunuo utujie, Watu ukweli wajue.

2. Yalete karibu Mataifa yote; Acha kila mtu Kanuni ashike. Mungu Baba, simamia Kwa takatifu sheria.

3. Utukufu wako, Wote wauone, Dunia iwepo Na waongofuwe. Libariki na Kanisa, Jaza dunia na wema.

4. Kwa Mungu pekee, Ndiye Mtukufu, Haleluya kwake Aishiye juu; Sifuni wote mlipo, Baba, Mwana, naye Roho.