1. Tumeitwa kumtumikia Mwenyezi tumshuhudie, Tuhubiri injili ya Bwana, Upendo tutangaze.
Mbele, kila mara, tumtukuze Bwana; Mbele, kila mara, tumtukuze Bwana; Mbele, twende mbele, ushindi tukiimba. Mungu ni nguvu, twendeni mbele Kutumikia.
2. Tumeitwa tujue baraka Sisi watoto wa Mfalme Na tunamwabudu kwa furaha, Twakiri jina lake.