1. Sote ni askari, dhambi tuzishinde; Tufurahi! Tufurahi! Taji la utukufu tutazamie; Tutalishinda taratibu. Hima vitani, kaza mwendo; Ukweli daima ni ngao. Ona bendera ivumavyo! Kwa shangwe, shangwe twarudi kwetu.
Sote ni askari dhambi tuzishinde; Tufurahi! Tufurahi! Taji la utukufu tutazamie; Tutalishinda taratibu.
2. Sikia! Mbiu yalia kwa sauti; Itikia! Itikia! Tunasubiri askari; U tayari? Msalabani kusanyika. Aita Jemedari wetu; Usichelewe, usihofu! Pigania Mwokozi wetu; Kwa shangwe, shangwe twarudi kwetu.
Sote ni askari dhambi tuzishinde; Tufurahi! Tufurahi! Taji la utukufu tutazamie; Tutalishinda taratibu.
3. Tunapigania falme ya mbinguni; Tufurahi! Tufurahi! Twaimba twendavyo; kheri tu askari, Punde ushindi tutapata. Hatari zaja – Je, tuhofu? Kiongozi daima, Yesu. Faraja, na Mlinzi wetu. Kwa shangwe, shangwe twarudi kwetu.
Sote ni askari dhambi tuzishinde; Tufurahi! Tufurahi! Taji la utukufu tutazamie; Tutalishinda taratibu.