Book cover

Tunasimama Sayuni

Nyimbo za Dini, 148


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Tunasimama Sayuni Vijana shupavu, Ahadi yatung’aria, Wajibu ni wetu, Msingi wa maadili Kuuendeleza. Twazimudu changamoto— Wakweli daima!

2. Ukweli tufuatao Wadharaulika. Lakini tunapotii Twajua twaweza Kuyahimili maovu Yaangamizayo. Tunayo fimbo ya chuma, Furaha ilimo.

3. Hofu na jaribu huja, Ila hatuhofu. Ni kwa ajili ya haki Tunauthubutu. Tutapenda, tutashinda; Wimbo tutaimba Kama vijana Sayuni— Wasafi, imara.