1. Sikilizeni, mataifa! Shangilieni kwa pamoja, Malaika imbeni wimbo: Nuru tena ipo!
Injili, mwanga wa ukweli, Wan’gara kutoka mbinguni, Ni mng’aavu kama jua Kote waangaza.
2. Watu walisaka gizani, Wakakesha wakisubiri. Sasa usiku umekwisha, Nuru yarejeshwa!
Injili, mwanga wa ukweli, Wan’gara kutoka mbinguni, Ni mng’aavu kama jua Kote waangaza.
3. Tumeitwa na Mungu wetu , Kutumikia wote watu, Tutasimamia ukweli, Neno kuhubiri.