1. Labda siyo kwenye milima Wala penye tufani, Labda siyo mbele ya vita Bwana anihitaji. Akiniita, kwa upole Nipite njia mpya, Nitajibu, Bwana, Mwaminifu: Utakako, nitakwenda.
Nitakwenda utakako, Bwana, Milimani hata ng’ambo; Nitasema utakacho, Bwana; Nitakuwa utakavyo.
2. Labda leo kuna maneno Natakiwa niseme; Labda kwenye njia za dhambi Yupo asumbukaye. Mwokozi wangu, niongoze, Njiani penye giza, Ili nitangaze neno tamu; Utakacho, nitasema.
Nitakwenda utakako, Bwana, Milimani hata ng’ambo; Nitasema utakacho, Bwana; Nitakuwa utakavyo.
3. Kuna mahali duni hasa Huko kwa walimwengu Pa kwenda kufanyia kazi Kwa ajili ya Yesu. Hivyo najikabidhi kwako, Nikijua napendwa, Hili nafanya kwa moyo wote: Utakavyo, nitakuwa.
Nitakwenda utakako, Bwana, Milimani hata ng’ambo; Nitasema utakacho, Bwana; Nitakuwa utakavyo.