1. Kwa Nefi, mwonaji yule, Mungu kafunua, Mfano wa neno lake Ni fimbo ya chuma.
Ishike fimbo ya chuma; Aminifu kweli. Hii fimbo— neno la Bwana— Mwongozo thabiti.
2. Tupo bado safarini, Kwenye majaribu; Tutapitia gizani, Penye hatari tu.
Ishike fimbo ya chuma; Aminifu kweli. Hii fimbo— neno la Bwana— Mwongozo thabiti.
3. Adui akisogea, Kutisha njiani, Tushike fimbo ya chuma, Tuombe auni.
Ishike fimbo ya chuma; Aminifu kweli. Hii fimbo— neno la Bwana— Mwongozo thabiti.
4. Hatua na kwa hatua, Siku hadi siku, Kwa sala na wimbo pia, Tusonge mbele tu.
Ishike fimbo ya chuma; Aminifu kweli. Hii fimbo— neno la Bwana— Mwongozo thabiti.
5. Pumziko li karibu, Yaongoza fimbo, Tutapata utukufu Tukishika neno.