1. Twalipenda neno lako Likihubiriwa. Hutuinua mioyo Ili kutukuza.
2. Twapenda kusoma neno Kwa wazo na sala. Anatuongoza Roho; Twahisi kulindwa.
3. Twapenda kuitangaza Injili ya Kristo. Twapeana ushuhuda Wa wokovu wako.
4. Twakushukuru kwa neno; Kwa nyimbo twasifu. Tupe uelewa, Kristo, Tuwe watiifu.