Book cover

Mahekalu ya Sayuni

Nyimbo za Dini, 162


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Mahekalu ya SayuniYang’ara utukufu,Njia ya kwenda mbinguni,Alama ya uungu.Taswira ya kuvutiaYatuita kuomba;Watiifu wa ahadi,Pale tutatumika.

2. Mungu Baba wa rehema,Tutakase twaomba;Bariki dhamira yetuYa ndugu kuokoa,Hadi siku watiifu,Wote tuliofungwaKwa pingu za selestia,Tuziimbe hosana.

3. Mbingu, imba kwa sauti,Nyimbo za kumsifuMfalme Imanueli!Imba Watakatifu!Milima ishangilieNa konde zifurahi,Nyota nazo zimsifuAmeshinda kaburi.