1. Baba yangu, uishiyePalipo patukufu,Lini nitarudi kwako,Na tena nisujudu?Je, kwako patakatifu,Niliishi kiroho?Asili yangu ya kwanza,Nililelewa kwako?
2. Kwa kusudi la pekeeNaishi duniani,Na bila ya kumbukumbuYa wangu uasili;Kuna muda nasikiaNong’ono, “Sio kwenu,”Na nahisi natokeaMahali patukufu.
3. Kupitia Roho wako,Nilikuita Baba.Hadi kurejeshwa nuruSababu sikujua.Mbinguni kuna Baba tu?Maana haileti!Kweli ni mantiki; kweliNina mama mbinguni.
4. Niiachapo dunia,Mwili niulazapo,Baba, Mama, mtaachaNiwaone mliko?Basi nikishamalizaKufanya kazi zote,Ikiwa mtakubali,Ruhusu kwenu nije.