Book cover

Nyumbani ni Mbinguni

Nyimbo za Dini, 168


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Nyumbani ni mbinguni, Pakiwa na pendo, Huleta shangwe nyingi, Baraka za Kristo— Amani na hisani, Usalama, ulinzi— Hufanya nyumbani kuwa Kama mbinguni.

2. Familia pamoja, Huwa na amani, Kutumiwa na Mungu, Twakua nuruni. Wazazi hufundisha, Watoto hufuata, Kupafikia mbinguni, Tutapo kuwa.

3. Kusali kila siku, Tutahisi pendo, Kusoma neno lake, Twastawisha moyo, Kwa nyimbo tutaomba, “Utuonyeshe, Baba, Njia ya kufika kwako, Tutapo kuwa.”