1. Dada wa Sayuni, tushirikiane Baraka za Mungu kuzitafuta. Kwa nguvu tuujenge ufalme wake, Kwa wale wanyonge tuwe faraja.
2. Tumepewa ujumbe wa malaika, Na twajivunia kipawa hiki: Tufanye vyote vya utu kwa pamoja Kwa jina la huruma tubariki.
3. Azima na wito wetu ni mpana, Kazi za kiroho tutekeleze. Ni Roho tu atakayetufundisha Tupate hekima tufanikiwe.