1. Watoto wa Mungu na wenye ukuhani, Mueneze neno na mkusanye watu. Sasa imeanza kazi, Wakusanye Israeli, Na warudi Sayuni kumsifu.
2. Njooni kondoo, msikilize Bwana, Mvune baraka zilizotabiriwa Na manabii wa kale, Kwamba mtaishi naye Awalete Sayuni mumsifu.
3. Tubu, mbatizwe na mtasamehewa, Mumpate Roho, muwe kitu kimoja. Muombeni msamaha; Naye atajibu sala Na mrudi Sayuni kumsifu.
4. Yatakapokwisha majonzi na mateso, Roho zitaenda kungoja Ufufuo; Na mtakaa pamoja, Mbinguni kwenye furaha, Mtakaa Sayuni kumsifu.