Book cover

Vyote Vyenye Uzuri

Nyimbo za Dini, 173

1. Kwa kila ua dogo, Ndege wa kuimba, Kawapa rangi nzuri, Kawapa na mbawa.

Vyote vyenye uzuri, Miti na wanyama, Vyote vyenye fahari Bwana kaviumba.

2. Kilele cha mlima, Mto wamwagika, Jua lichomozapo Huangaza anga.

Vyote vyenye uzuri, Miti na wanyama, Vyote vyenye fahari Bwana kaviumba.

3. Upepo wa baridi, Kiangazi chema, Matunda bustanini, Kayatengeneza.

Vyote vyenye uzuri, Miti na wanyama, Vyote vyenye fahari Bwana kaviumba.

4. Miti yenye kijani, Konde zavutia, Kando kando ya maji Tunakusanyika.