November 2019
Naenda Na Yesu
Naenda Na Yesu
1. Yesu alikua,
Nayo hekima,
Na upendo kwa watu kaonyesha.
Anielekeza,
Njia nipate,
Akiniita nitembee naye.
Naenda na Yesu Mbinguni huko,
Bwana atanibariki, Niwe na upendo.
Anibadilisha; Nipate maoni.
Naenda na Yesu, Ataenda nami.
2. Nitamwiga Yesu.
Nitajaribu
Kuzitii amri kila siku.
Nitakaa naye
Akinilinda,
Nitakuwa naye kumtangaza.
Naenda na Yesu Mbinguni huko,
Bwana atanibariki, Niwe na upendo.
Anibadilisha; Nipate maoni.
Naenda na Yesu, Ataenda nami.
3. Nitamuamini;
Nitaitika.
Hataniacha hata nikikosa.
Ananipa nguvu,
Anifariji,
Milele nikikua na kuishi.
Naenda na Yesu Mbinguni huko,
Bwana atanibariki, Niwe na upendo.
Anibadilisha; Nipate maoni.
Naenda na Yesu, Ataenda nami.
Maandishi na muziki: Stephen P. Schank, kuz. 1967
©2019 by Intellectual Reserve, Inc. All rights reserved. Wimbo huu wa dini ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani. Notisi hii lazima ionekane kwenye kila nakala iliyotolewa.