September 2021, page 13
Ndiye Amani
Ndiye Amani
1. Ndiye amani
Mwokozi wetu.
Hisi upendo wake
Kutunusuru.
Maneno yake.
Yawe uhai.
Kama tutatambua,
Ndiye amani.
Anatupa
Pumziko.
Nguvu yetu
Tuzidiwapo.
Hifadhi yetu
Penye hatari.
Penye hofu kuu,
Ndiye amani.
2. Ndiye amani
Njiani kwetu
Galilaya,na pia
Yerusalemu.
Ponya mioyo
Futa Machozi.
Tuishi kama yeye.
Ndiye amani.
Anatupa
Pumziko.
Nguvu yetu
Tuzidiwapo.
Hifadhi yetu
Penye hatari.
Penye hofu kuu,
Ndiye amani,
Penye hofu kuu,
Ndiye amani.
Maneno na muziki na Nik Day
© 2021 by Intellectual Reserve, Inc. All rights reserved. Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani. Notisi hii lazima ionekane kwenye kila nakala iliyotolewa.