Nyimbo Za Dini Pamoja Na Nyimbo Za Watot (1983),
p. 3
Mkombozi Wa Israel
Mkombozi Wa Israel
1. Mwokozi wa Israeli, nuru yetu,Tunayemwomba baraka,Kivuli mchana; nguzo usiku,Mfalme, mwingine hatuna!
2. Twajua aja kukusanya kondooAwaongoze Sayuni;Wasilie kwenye bonde la kifoNa wasizurure nyikani.
3. Tumetangatanga sana kwenye dhambi,Jangwani tukakuomba!Adui wabeza yetu majonzi,Lakini huru tutakuwa.
4. Habari njema kwetu wana Sayuni.Ishara zaonekana.Kwani ufalme ni wetu, tutii.Saa ya ukombozi yaja.
5. Nirejeshee, Mwokozi, nuru yako;Faraja ya roho nipe;Na ile shauku ya kuja kwakoMoyo tumaini iipe.
6. Atazama! Na malaika wasifu,Wengi neno wangojea;Anena! Na anga zote za juu,Zazijibu sifa za Bwana.
Maandishi: William W. Phelps, 1792–1872; yamefanyiwa marekebisho kutoka kwa Joseph Swain, 1761–1796. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.
Muziki: Freeman Lewis, 1780–1859