Nyimbo Za Dini Pamoja Na Nyimbo Za Watot (1983),
p. 36
Najua Mwokozi Wangu Anaishi
Najua Mwokozi Wangu Anaishi
1. Najua Kristo Yu hai.Neno hili hufariji!Yu hai, aliyekufa.Yu hai kuniongoza.Yu hai, Neema yetu.Yu hai, Wakili wangu.Yu hai anistawishe.Yu hai, Uzima ndiye.
2. Yu hai kuniwezesha.Yu hai kunifundisha.Yu hai kunipa nguvu.Yu hai nafsi kutibu.Yu hai, niwe jasiri.Yu hai kufuta chozi.Yu hai moyo apoze.Yu hai nibarikiwe.
3. Yu hai Rafiki mwema.Yu hai na anipenda.Yu hai, niimbe hivi.Yu hai wangu Nabii.Yu hai, pumzi iwepo.Yu hai nishinde kifo.Yu hai, mbinguni niwe.Yu hai, nifike kwake.
4. Yu hai! Ni mtukufu!Yu hai Mwokozi wangu.Neno hili hufariji:“Najua Kristo yu hai!”Yu hai! Ni mtukufu!Yu hai, Mwokozi wangu.Neno hili hufariji:“Najua Kristo yu hai!”
Maandishi: Samuel Medley, 1738–1799. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.
Muziki: Lewis D. Edwards, 1858–1921
Maandishi: Samuel Medley, 1738–1799. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.