Page 52
Sifa Kwake Yeye
Sifa Kwake Yeye
1. Sifa kwa aliyenena na Bwana!Nabii huyo alitawazwa.Alifungua kipindi cha mwisho,Watamheshimu mataifa.
Shangwe kwa nabii kwenda mbinguni!Waasi sasa, bure wapinga.Akichangamana nao Miungu;Na kifo hakimshindi tena.
2. Atakumbukwa kwa kufia dini;Jina lake litaheshimiwa!Damu waliyoimwaga waovu,Kwake Mungu itamtetea.
Shangwe kwa nabii kwenda mbinguni!Waasi sasa, bure wapinga.Akichangamana nao Miungu;Na kifo hakimshindi tena.
3. Hauna mwisho ukuhani wake.Milele funguo amiliki.Ataingia katika ufalme,Kutuzwa kati ya manabii.
Shangwe kwa nabii kwenda mbinguni!Waasi sasa, bure wapinga.Akichangamana nao Miungu;Na kifo hakimshindi tena.
4. Dhabihu yatuletea baraka.Kote maovu yatajutiwa.Zindukeni tupiganie haki.Jina la Joseph litakumbukwa.
Shangwe kwa nabii kwenda mbinguni!Waasi sasa, bure wapinga.Akichangamana nao Miungu;Na kifo hakimshindi tena.
Maandishi: William W. Phelps, 1792–1872
Muziki: Wimbo wenye asili ya Uskoti