1. Asubuhi kunakucha;
Ona, bendera Sayuni!
Pambazuko siku ng’avu,
Pambazuko siku ng’avu
Yaja humu duniani.
2. Ukiangaza ukweli
Wingu la giza huisha,
Utukufu toka mbali,
Utukufu toka mbali
Waangaza mataifa.
3. Injili kamili yaja,
Baraka kwa Israeli,
Yuda dhambi watakaswa,
Yuda dhambi watakaswa,
Wairithi Kaanani.
4. Yehova anaongea,
Wayunani sikiliza.
Mkono wake u wazi,
Mkono wake u wazi
Wateule kupokea.
5. Malaika toka juu
Wameweka ushahidi;
Na Sayuni yaangaza,
Na Sayuni yaangaza
Kuleta Wema nyumbani.
Maadishi: Parley P. Pratt, 1807–1857
Muziki: George Careless, 1839–1932