Number 5
Juu ya Mlima
Juu ya Mlima
1. Juu ya mlimaBendera ilipo,Mataifa, ona;Ipeperukavyo.Ni katika Desereti,Kwenye mlima Sayuni!
2. Mungu akumbukaAhadi za kale,Juu ya mlimaKweli zifunguke!Mwanga wake kivutioKwa wote siku za mwisho.
3. Nyumba itajengwa,Yenye utukufu,Semi zitakuwaKutoka kwa watu:Twende kwake tujifunze,Na tutii amri zake.
4. Huko tutafunzwaSheria za kweli,Na zitatawalaKote duniani.Tufuate njia zake,Ili sote tuokoke.
Maandishi: Joel H. Johnson, 1802–1882
Muziki: Ebenezer Beesley, 1840–1906