Book cover

Kwa Milima Twakutukuza

Nyimbo za Dini, 8

0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Kwa milima twakutukuza Ewe, Mungu wetu; Unatuwezesha sana Katika kazi zetu. Waileta Israeli Kwenye nchi yao.

Kwa milima twakutukuza, Ewe, Mungu wetu.

2. Mikononi mwa waonevu Tumenyanyasika; Umekuwa msaada Wa kutuimarisha, Tukapita maadui Katikati yao.

Kwa milima twakutukuza, Ewe, Mungu wetu.

3. Umetuongoza salama Hadi kwenye kinga Ukiwa mlinzi wetu Tangu tulikotoka. Kwa ajili ya miamba, Mabonde, na mito,

Kwa milima twakutukuza, Ewe, Mungu wetu.

4. Sisi twauchunga mnara Nuru isizime; Sisi ni waangalizi Chini ya anga kete. Miamba yajasirisha, Kwa ya kwako fimbo;

Kwa milima twakutukuza, Ewe, Mungu wetu.