Number 8
Kwa Milima Twakutukuza
Kwa Milima Twakutukuza
1. Kwa milima twakutukuza
Ewe, Mungu wetu;
Unatuwezesha sana
Katika kazi zetu.
Waileta Israeli
Kwenye nchi yao.
Kwa milima twakutukuza,
Ewe, Mungu wetu.
2. Mikononi mwa waonevu
Tumenyanyasika;
Umekuwa msaada
Wa kutuimarisha,
Tukapita maadui
Katikati yao.
Kwa milima twakutukuza,
Ewe, Mungu wetu.
3. Umetuongoza salama
Hadi kwenye kinga
Ukiwa mlinzi wetu
Tangu tulikotoka.
Kwa ajili ya miamba,
Mabonde, na mito,
Kwa milima twakutukuza,
Ewe, Mungu wetu.
4. Sisi twauchunga mnara
Nuru isizime;
Sisi ni waangalizi
Chini ya anga kete.
Miamba yajasirisha,
Kwa ya kwako fimbo;
Kwa milima twakutukuza,
Ewe, Mungu wetu.
Maandishi: Felicia D. Hemans, 1793–1835; yamefanyiwa marekebisho na Edward L. Sloan, 1830–1874
Muziki: Evan Stephens, 1854–1930