Number 23
Sayuni Nzuri Mbinguni
Sayuni Nzuri Mbinguni
1. Sayuni nzuri mbinguni;Napenda mji mzuri;Mizuri milango yake;Hekalu – Mungu nuruye;Aliyenipatanisha,Milango aifungua.
A! Sayuni, ni kuzuri;Mji Sayuni;Sayuni, kwake Mungu!
2. Kuzuri mbinguni kote;Hata malaika wote;Nzuri nazo tumbuizo;Nzuri tarumbeta zao;Nitaimba na umati,Miguuni pa Mwokozi.
A! Sayuni, ni kuzuri;Mji Sayuni;Sayuni, kwake Mungu!
3. Mazuri mataji yao,Matawi watandazayo;Wazuri wakombolewa,Wote wanaoingia;Nitaingia kwa hamuKwenye pumziko langu.
A! Sayuni, ni kuzuri;Mji Sayuni;Sayuni, kwake Mungu!
Maandishi: George Gill, 1820–1880
Muziki: Joseph G. Fones, 1828–1906