Book cover

Utukufu na Sifa

Nyimbo za Dini, 30


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Utukufu na sifa Mfalme ni vyako, Wanao twakusifu Hosana kwa Kristo. Bwana wa Israeli, Mwana wa Daudi, Unayekuja Yesu, Kama Mkombozi.

2. Kundi la malaika Lakusifu juu, Navyo viumbe vyote Vyatoa majibu. Kama Waebrania Wabeba matawi, Tunakupa upendo Na sifa, Mwokozi.

3. Kabla ya kifo chako, Waliimba sifa; Sasa upo mbinguni, Twakusifu Bwana. Pokea sifa zetu, Na pendo la kweli, Kwako yote ni mema, Mfalme mzuri.