Number 30
Utukufu na Sifa
Utukufu na Sifa
1. Utukufu na sifa
Mfalme ni vyako,
Wanao twakusifu
Hosana kwa Kristo.
Bwana wa Israeli,
Mwana wa Daudi,
Unayekuja Yesu,
Kama Mkombozi.
2. Kundi la malaika
Lakusifu juu,
Navyo viumbe vyote
Vyatoa majibu.
Kama Waebrania
Wabeba matawi,
Tunakupa upendo
Na sifa, Mwokozi.
3. Kabla ya kifo chako,
Waliimba sifa;
Sasa upo mbinguni,
Twakusifu Bwana.
Pokea sifa zetu,
Na pendo la kweli,
Kwako yote ni mema,
Mfalme mzuri.
Maandishi: Theodulph wa Orleans, 760–821
Muziki: Melchior Teschner, 1584–1635